TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, April 17, 2012

Iddi Seif Sandaly Rais Mpya Wa Chama Cha Watanzania DMV

12:44 PM

Iddi Seif Sandaly ndiye rais mpya aliyechaguliwa kwenye mkutano wa uchaguzi wa Watanzania DMV uliofanyika katika ukumbi wa Mirage, Iddi Seif Sandaly alishinda kwa kura 205.
Jacop Kinyemi aliyekuwa kwenye kinyang'anyiro cha Ukatibu Mkuu na kuwa wa pili kwa kura 82, Amos Cherehani ndiye aliyeshinda Ukatibu Mkuu kwa kura 192 na Rhoda Kasamba kwenye nafasi ya Ukatibu Mkuu alipata kura 40.
Loveness Edwin Mamuya ambaye alikuwa mgombea wa Urais kwenye mkutano wa uchaguzi uliofanyika Jumapili Aprili 15, 2012 na kupata kura 119.
 Mselem (kushoto) na Dr. Mwamoyo Hamza, Kamati ya Kurekebisha Katiba ambayo pia ilisimamia uchaguzi wakitayarisha vitendea kazi na kuweka mambo sawa kabla ya upigaji kura.
 Mgombea Uraisi Loveness Mamuya (kati) akifuatilia mkutano wa uchaguzi
Maafisa Ubalozi wakifuatilia uchaguzi huo.
 Watanzania wa DMV wakiwa mkutanoni.
 Watanzania wa DMV ambao Jumapili Aprili 15, 2012 walifika kwa wingi na kuandika historia mpya kwa kuwachagua viongozi watakaoongoza Jumuiya DMV ambayo ilikuwa inalegalega tangia 2007.
 Mgombea wa Urais Iddi Sandaly (kati) akifuatilia mkutano wa uchaguzi.
Wajumbe wa Bodi ambao wote walipita kwenye uchaguzi huo kutoka kushoto ni Al- Amini Chande, Dr. Hamza Mwamoyo, Eliserena Kimolo, Grace Sebo Mgaza na Haruni Ulotu.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA