Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mpango wa kuanzisha bednki ya Jamii ya Muwape Saccos Mtemani Wete Pemba, alipokuwa katika ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za Kijamii Mkoani humo,(kulia) Mize Khamis.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumpokea katika uwanja wa karume Pemba alipowasili kisiwani humo kwaziara maalum kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za kijamii.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mtoto Suleiman Shaaban Juma,pamoja na wanachama wa Kampuni ya Mkipi Miliki Tungamaa,kuzindua Mradi wa uzalishaji wa sabuni kwa kutumia mashine maalum ya Mkipi Miliki,jana akiwa katika ziara kisiwani Pemba,kuangalia maendeleo ya jamii.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na watendaji wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za Mkoa huo,katika ukumbi wa Jamhuri Hall Wete Pemba jana,(kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Hamadi Mberwa Hamadi,na (kushoto) Mkuu wa Mkoa huo Dadi Faki Dadi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein,akiangalia Sabuni iliyotengenezwa katika kampuni ya Mkipi Miliki Tungamaa,ambayo inayozalisha sabuni kwa kutumia mashine maalum,alipokuwa katika ziara ya kutembelea maendeleo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba,(kulia) Mkurugenzi Mkuu George M.Buchwafwe.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar
0 comments:
Post a Comment