TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, April 17, 2012

LULU ASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 17 GEREZANI JANA

12:46 PM

MSANII wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu' jana Jumatatu alitimiza miaka 17 akiwa katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.
Lulu, ambaye anashikiliwa katika gereza hilo akishtakiwa kwa madai ya kumuua msanii wa filamu Steven Kanumba, Jumatano iliyopita alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu, lakini hakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria kusikiliza kesi za mauaji.
Kwa mujibu wa cheti cha kuzaliwa ambacho Mwanaspoti imekiona, inaonyesha kuwa Lulu alizaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Aprili 16, mwaka 1995.
Hiyo ina maana kuwa jana Jumatatu, Lulu alisherehea siku yake ya kuzaliwa, ingawa hakuna uhakika kama �alikula keki� gerezani.
Cheti hicho kinaonyesha kuwa Lulu amesajiliwa kwa majina ya Diana Elizabeth, huku jina la baba likiwa ni Michael Edward Kimemeta na mama akiitwa Lucresia Agustino Kalugila.
Cheti hicho kinaonyesha kuwa Lulu alizaliwa Aprili 16, 1995, lakini alisajiliwa siku tatu baadaye, yaani Aprili 19, mwaka huo.
Lulu, ambaye alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jumatano iliyopita na kutotakiwa kujibu chochote, alitoa maelezo yake Polisi Jumatatu ya wiki iliyopita ikiwa ni saa 65 tangu kutokea kwa kifo cha Kanumba Aprili 7.
Lulu alizungumza na kachero wa Makao Makuu ya Polisi ambaye pia ana taaluma ya saikolojia.
Taarifa za uhakika ambazo Mwanaspoti limezipata kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa kachero huyo (jina tunalo) alitoka Makao Makuu kusaidia kufanya mahojiano na binti huyo ambaye mtoa taarifa wetu anasema hakuwa tayari kufanya hivyo kutokana na msongo wa mawazo, lakini alitumia takribani muda wa saa tatu kumlainisha Lulu.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA