Katibu
Mtendaji wa BASATA, Bw. Materego akisisitiza jambo wakati wa majumuisho
ya Jukwaa la Sanaa wiki hii. Kulia kwake ni Msanii Raza na Kaimu
Mratibu wa Jukwaa hilo. Bi. Agnes Kimwaga.
Mchoraji
maarufu nchini Mohamed Raza (Kulia) akionesha moja ya kazi zake wakati
akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu
makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Kulia kwake ni Katibu
Mtendaji wa BASATA, Bw. Ghonche Materego.
Mdau
Joshuia ambaye ni msanii wa Sanaa za Ufundi akichangia mada kwenye
Jukwaa la Sanaa wiki hii. Alishauri wilaya ziwe na eneo maalum la
maonyesho ya kazi za mikono.
==== ===== =======
Na Ripota Wetu Jijini.
Wadau
wa Sanaa wameiomba serikali kutumia balozi zake zilizoko kwenye mataifa
mbalimbali duniani kutangaza kazi za wasanii nchini ili kuweza kutanua
masoko yao.
Ombi
hilo limetolewa wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa wakati msanii maarufu
wa sanaa za uchoraji nchini, Mohamed Raza alipokuwa akiwasilisha mada
kuhusu ‘Mchango wa Sanaa za Ufundi Katika Soko la Utalii’ ambapo
alisema kwamba, kuna kila sababu ya serikali kuwa na kitengo maalum
katika balozi kinachohusika na kutangaza kazi za wasanii wa ndani.
“Inabidi
tutumie balozi zetu za nje kutangaza kazi za wasanii. Balozi za wenzetu
hapa nchini zimekuwa zikifanya kazi ya kutangaza bidhaa za wasanii wao
hapa kwetu na sisi lazima tufanye hivyo na tushirikiane nao” alisema
Raza ambaye amepata bahati ya kuchora picha za marais wote wa nchi hii.
Aliongeza
kwamba, wasanii hapa nchini wamekuwa wakitengeneza kazi nyingi zenye
ubora hasa za ufundi lakini tatizo kubwa limekuwa kwenye masoko hasa
ya nje na kuongeza kwamba, kwa balozi kuwa na eneo maalum la kuonesha
kazi za wasanii kutasaidia sana kutanua soko.
Wadau
wengine waliochangia mjadala huo, waliiomba serikali kutilia mkazo
matumizi ya kazi za sanaa za ufundi katika ofisi zake ili kutanua soko
la wasanii wa ndani badala ya ilivyo sasa ambapo kumekuwa na uagizaji
wa bidhaa hizo kutoka nje.
“Vijana
wengi sana wamejiajiri kwenye sekta ya sanaa na hata kwenye pato la
taifa wamekuwa wakichangia lakini tatizo ni kutothaminiwa kwa kazi zao.
Serikali iwe mstari wa mbele kuthamini kazi za wasanii na kuzitumia
katika ofisi zake” alishauri Joshua mbaye ni moja ya wasanii wa Sanaa
za Ufundi nchini.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego alisema kwamba,
Serikali imekuwa ikiwathamini wasanii wake ndiyo maana imekuwa
ikishirikiana nao katika kazi mbalimbali yakiwemo matukio ya kitaifa.
“Makatibu
Wakuu wa wizara kupitia kikao chao, wamelitaka Baraza kukusanya wasanii
wachoraji kwa ajili ya kuchora nembo ya miaka 50 ya uhuru. Baraza
limefanya hivyo kwa kushirikiana na Shirikisho la Sanaa za Ufundi.
Mtaona ni kwa jinsi gani wasanii wamekuwa wakipewa nafasi kubwa”
alisema Materego.
0 comments:
Post a Comment