Na Mwandishi Wetu, Loliondo
Tiba ya kikombe inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile ni balaa, mvuto wake unaitikisa dunia na hivi sasa Wahindi na Wazungu wamejaa Kijiji cha Samunge, Loliondo kupata huduma hiyo.
Uchunguzi wa Risasi Mchanganyiko ‘The 5star Paper’ umebaini kuwa, Wazungu, Wahindi na raia wengine wa kigeni wanaendelea kumiminika Loliondo kutokana na ripoti wanazopata.
Gazeti
hili limebaini kuwa, vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa
vimekuwa vikiripoti kuhusu miujiza ya Babu wa Loliondo, hivyo kutoa
hamasa kwa watu wa mataifa kuja nchini kupata kikombe cha tiba.
Wiki iliyopita, Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani ya Radio Deutsche Welle (DW) ambayo husikika dunia nzima, ilitoa makala maalum inayoelezea tiba ya Babu Ambi wa Loliondo.
Mbali na DW, mashirika mengine ya habari ya kimataifa ambayo kwa nyakati tofauti yamekuwa yakiripoti kuhusu miujiza ya Babu ni BBC na VOA, zote kupitia idhaa zake za Kiswahili.
Vyombo hivyo vya habari vimeupaisha umaarufu wa Babu kiasi cha raia wengi wa kigeni kutamani kufika kumuona kwa macho ‘mganga’ huyo aliyedai kuoteshwa dawa hiyo na Mungu.
Uchunguzi unaonesha kwamba, mpaka sasa raia zaidi ya 3,000 wa kigeni wameshafika kwa Babu na kupata kikombe cha dawa huku wengine wakiwa wanaulizia njia ya kufika wakiwa jijini Arusha.
Gazeti
hili limebaini kuwa, watu 70 kutoka barani Ulaya wameshapata kikombe
cha Babu, wakati Wahindi wameendelea kuzagaa Samunge utadhani ndipo
yalipo makazi yao ya siku zote.
Kwa muda mrefu sasa, Wahindi wamekuwa wengi Loliondo tangu tiba hiyo ya miujiza ilipopata umaarufu mwishoni mwa Februari, mwaka huu huku baadhi yao wakitoa huduma kama wasaidizi wa mzee huyo.
Takwimu zilizokusanywa katika eneo la utoaji wa dawa zinaonesha kuwa, wageni kutoka nchi jirani ya Kenya ndiyo wanaoongoza kwa kunywa dawa hiyo.
Mpaka sasa, zaidi ya Wakenya 2,400 wameripotiwa kupata kikombe cha Babu.
Nchi nyingine ambazo raia wake wameshafika kijijini Samunge na kunywa dawa hiyo ni Marekani, Finland, Uholanzi, Siri Lanka, Jumuiya ya Falme za Kiarabu (UAE), Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Uganda, Rwanda, Burundi na Comoro.
Kutokana
na wingi wa wageni hao, tayari ilisharipotiwa kuwa, Idara ya Uhamiaji,
imepiga kambi kijijini Samunge ili kupitia nyaraka mbalimbali za wageni
wanaoingia.
Jina la Babu limekuwa likivuka mipaka kutokana na sifa yake kubwa kwamba dawa yake ya miujiza, inatibu magonjwa sugu, yakiwemo shinikizo la damu, ukimwi, kisukari, kifafa na pumu.
Hata hivyo, siku za karibuni kumeanza kuzuka hoja mbalimbali, nyingine kutoka kwenye uongozi wa makanisa kwamba, dawa ya Babu haina baraka za Mungu au haiponyi.
Tiba ya kikombe inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile ni balaa, mvuto wake unaitikisa dunia na hivi sasa Wahindi na Wazungu wamejaa Kijiji cha Samunge, Loliondo kupata huduma hiyo.
Uchunguzi wa Risasi Mchanganyiko ‘The 5star Paper’ umebaini kuwa, Wazungu, Wahindi na raia wengine wa kigeni wanaendelea kumiminika Loliondo kutokana na ripoti wanazopata.
Wiki iliyopita, Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani ya Radio Deutsche Welle (DW) ambayo husikika dunia nzima, ilitoa makala maalum inayoelezea tiba ya Babu Ambi wa Loliondo.
Mbali na DW, mashirika mengine ya habari ya kimataifa ambayo kwa nyakati tofauti yamekuwa yakiripoti kuhusu miujiza ya Babu ni BBC na VOA, zote kupitia idhaa zake za Kiswahili.
Vyombo hivyo vya habari vimeupaisha umaarufu wa Babu kiasi cha raia wengi wa kigeni kutamani kufika kumuona kwa macho ‘mganga’ huyo aliyedai kuoteshwa dawa hiyo na Mungu.
Uchunguzi unaonesha kwamba, mpaka sasa raia zaidi ya 3,000 wa kigeni wameshafika kwa Babu na kupata kikombe cha dawa huku wengine wakiwa wanaulizia njia ya kufika wakiwa jijini Arusha.
Kwa muda mrefu sasa, Wahindi wamekuwa wengi Loliondo tangu tiba hiyo ya miujiza ilipopata umaarufu mwishoni mwa Februari, mwaka huu huku baadhi yao wakitoa huduma kama wasaidizi wa mzee huyo.
Takwimu zilizokusanywa katika eneo la utoaji wa dawa zinaonesha kuwa, wageni kutoka nchi jirani ya Kenya ndiyo wanaoongoza kwa kunywa dawa hiyo.
Mpaka sasa, zaidi ya Wakenya 2,400 wameripotiwa kupata kikombe cha Babu.
Nchi nyingine ambazo raia wake wameshafika kijijini Samunge na kunywa dawa hiyo ni Marekani, Finland, Uholanzi, Siri Lanka, Jumuiya ya Falme za Kiarabu (UAE), Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Uganda, Rwanda, Burundi na Comoro.
Jina la Babu limekuwa likivuka mipaka kutokana na sifa yake kubwa kwamba dawa yake ya miujiza, inatibu magonjwa sugu, yakiwemo shinikizo la damu, ukimwi, kisukari, kifafa na pumu.
Hata hivyo, siku za karibuni kumeanza kuzuka hoja mbalimbali, nyingine kutoka kwenye uongozi wa makanisa kwamba, dawa ya Babu haina baraka za Mungu au haiponyi.
0 comments:
Post a Comment