TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, April 16, 2011

MTOTO WA MIEZI 15 AHUDUMIWA KILEVI KWA BAHATI MBAYA…!!!

4:48 PM
Wazazi wa mtoto wa miezi 15 Dominic Lacey Wilson kutoka jimbo la Michigan nchini Marekani aliyehudumiwa pombe kwa bahati mbaya katika mgahawa wa Applebee wiki iliyopita, wamefungua jalada la kesi dhidi ya kampuni miliki ya mgahawa huo kutokana na tukio hilo wakidai fidia.

Wazazi hao Taylor Dill-Reese na Dominic Wilson wamefungua kesi hiyo katika mahakama ya Oakland ambako ndiko ulipo mgahawa huo, wakilalamika kuwa walipatwa na msongo kufuatia tukio hilo na kudai kupata hasara ya fedha kwa ajili ya matibabu ya motto huyo.

Ijumaa iliyopita familia hiyo ilitembelea katika mgahawa wa Applebees uliopo Madison Heights ambapo pamoja na mambo mengine waliagiza chakula cha mtoto kwa ajili ya Dominic ambacho kingekwenda sambamba na juisi ya epo.

Badala yake kinyaji alicholetea mtoto huyo ni margarita yenye kilevi ambapo baada ya kunywa mtoto huyo alianza kufanya vitendo vya ajabu vilivyopelekea wazazi wake kushangaa kwa kuwa sio kawaida yake.

Alipopelekwa katika hospitali ya karibu damu yake iligundulika kuwa na kilevi kiwango cha 0.10, ambacho ni kikubwa kuliko kiwango kilichowekwa na mamlaka ya Michigan kwa madereva cha 0.08. Mtoto huyo pia alipatwa na maumivu ya kichwa, mafua na mning’inio (hangover) kwa siku kadhaa baada ya tukio hilo.

Mwanasheria wa familia hiyo William Stern amesema hii sio mara ya kwanza kwa mgahawa huo kuchanganya vinywaji na pombe kwa watoto.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA