Na Mwandishi Wetu
BENKI
ya Exim Tanzania imeongeza faida ya pato lake kufikia sh. bilioni
16.6/-hadi mwishoni mwa mwaka jana ikiwa ni ongezeko la 66.7%
ukilinganisha na pato la sh. bilioni 9.99 la mwaka wa fedha 2009.
Mafanikio
hayo yanaifanya benki hiyo kuwa kinara wa ongezeko la faida katikasekta
ya kibenki nchini inayoonyesha kukua kwa kasi katika ufanisi na
ubunifukatika utendaji wake.Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa na benki hiyo jana nakusainiwa na Meneja Mkuu Dinesh Arora,
hatua hiyo ya maendeleo ya kasi inatokanana ushirikiano mzuri kiutendaji
uliojengekana miongoni mwa wadau wa benki hiyo.
“Tumeongeza
pato letu kwa 66.7% na kufika sh. bilioni 16.6 hadi ilipofikiamwishoni
mwa mwaka jana kutoka sh. bilioni 9.99 za mwaka 2009, hivyo ni hatua
yakupongezwa”, ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa
hiyo inaeleza faida ya uendeshaji wa benki kwa mwaka wa fedha
2010imeongezeka kwa asilimia 60% na kufikia shilingi 23.22 bilioni dhidi
ya shilingibilioni 13.87 ukitoa pato la ziada la shilingi bilioni 4
lililopatikana mwishomwa mwaka 2009.Inafafanua kuwa pato la benki kwa
ujumla limeongezeka kutoka sh.bilioni 127 nakufikia sh. bilioni 710
ilipofika mwishoni mwa Desemba 2010 na kuifanya Benki yaExim kuwa
miongoni mwa benki 6 kubwa nchini kuwa na rekodi nzuri katika pato
lajumla.Katika gawio la ‘gross NPA ratio’ benki ya exim imeshuka kufikia
4.1% ilipofikaDesemba 2010 kutoka 4.3% ya Desemba 2009.
Katika
kuendelea mbele, Benki ya Eximimeweka kipaumbele kwenye uongozi wa NPA
na kufanya tathimini ya kila marakatika kuhakikisha kitengo hicho
kinapanda kiubora.“Tumeonekana kushuka kidogo katika sehemu ya NPA
lakini benki inafanya jitihadaza makusudi kuhakikisha kuwa mikakati
mipya ya kusaidia kuinuka kwa kitengohicho inawekwa”, inasisitiza sehemu
ya taarifa hiyo.Benki ya Exim Tanzania ina matawi 22 katika sehemu
mbalimbali za nchi ikiwa nipamoja na kuwa na uendeshaji wa kibenki
katika Visiwa vya Comoro zinazoongozwana huduma ya ATM ambapo Tanzania
zipo 45 na 25 nje ya Tanzania. Katika kuhakikisha benki hiyo inaongeza
ufanisi wake kiutendaji, mwaka janaimeajiri wafanyakazi wengine 150
wakiwemo wataalamu watatu kutoka nje ya nchiikiwa ni kuendelea kuonyesha
mfano kwa kuwavutia watanzania waishio nje, kurudinyumbani na
kufanyakazi.
|
0 comments:
Post a Comment