Nguvu Kazi Gongo la Mboto na UhuruOne
Mdau Mihayo (kulia) na mafundi wakitandika batiNdugu yetu Ankal!
Wikiendi hii tulikwenda kuungana na ndugu zetu wa Gongo la Mboto kuona wapi tungeweza kushirikiana kupunguza makali ya maafa yaliowakumba. Tulipopata taarifa kwamba kuna shule 8 zimeathirika tukaona ni bora tuelekeze nguvu zetu huko ili wadogo zetu na walimu wao warudi kwenye hali ya kawaida haraka iwezekanavyo.
Basi tulikwenda kwenye shule ya sekondari ya Juhudi na kutathmini maafa yaliyowapata na Jumapili tulirudi tena na vifaa vya ujenzi na kuanza kuchapa kazi. Jumatatu tuliendelea na kazi na panapo maajaliwa leo tutakuwa tumemaliza kukarabati kuta zote, nguzo na kubadilisha mabati yote 12 yalioathirika.
Tunatanguliza shukurani kwa Mkuu wa Wilaya Mh. Leonidas Gama kwa kujiunga nasi kwenye nguvu kazi hii. Shukurani pia kwa Afisa Elimu wilaya na ofisi ya Mhandisi ya Wilaya kwa ushirikiano wao wa karibu na kwa mwenyeji wetu Mwl Mkuu tunamshukuru sana. Panapo maajaliwa tutarudi kumalizia kupaka rangi baada ya wiki.
Wako katika ujenzi wa Taifa
UhuruOne team.




0 comments:
Post a Comment