Msanii wa kikundi cha Taarab cha East African
Melody Bi Mwanahawa Ally ( 55) akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa wa
Morogoro leo baada ya kujeruhiwa kwenye ajali ya basi dogo la wasanii wa
Kundi la Five Stars Moden Taarab la Jijini Dar es Salaam. Yeye alikuwa
msanii mwalikwa kwenye safari hiyo ya kikazi katika mikoa ya nyanda za
juu kusini . Picha zote na habari na John Nditi wa Globu ya Jamii,
Morogoro
Majina
ya wanamuziki wa bendi ya Five Star Modern Taarab waliokufa katika
ajali ya gari Mikumi mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo yamefahamika.
Kwa
mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro Be.
Ibrahim Mwamakula, marehemu hao ni Issa Kijoti, Nasoro Madenge, Mapande,
Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall,Ngeleza Hasan,Hamisa
Omari,Maimuna , Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala
“ Hii ajali imepoteza watu 13 kati ya hao 12 wamefariki papo hapo na mmoja amefariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitalini.
"Ni
ajali mbaya kutokea iliyohusisha magari matatu, ambapo waliokufa wote
ni kutoka kwenye basi dogo la wasanii wa kikundi cha Five Stars na
kusababisha majeruhu tisa kulazwa” alisema Mwamakula, akifafanua kuwa
kati ya waliokufa 10 ni wanaume na watatu ni wanawake.
Amesema majeruhi tisa ambao wote ni wasanii waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ni pamoja na Mwanahawaa Ally( 55) kutoka Kundi la East African Melody, ambaye alikuwa ni msanii mwalikwa, Susana Benedict(32), Zena Mohamed (27), Samila Rajab (22)na Mwanahawa Hamisi (36)ambao wamelazwa wodi namba tatu.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliwataja wasanii wengine waliolazwa katika Hospitali hiyo ni pamoja na Ally Juma (25), Rajabu Kondo ( 25), Issa Hamis , Shaaban Hamis (41) na Msafiri Musa (22).
Kwa
mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa
Morogoro, kuwa dereva huyo aliligonga lori hiyo wakati akijaribu
kulikwepa Lori jingine lililokuwa likotokea mbele yake lenye namba T 530
BHY lenye tela T 182 BKB aina ya Scania ambapo katika harakati hizo
basi hilo lililigonga Lori hiyo mbele pembezoni na kusababisha magari
hayo kuanguka.
Alisema kuwa baada ya kuliparamia Lori hiyo , basi
hilo liliyumba na kuhama uoande wake na kujibamiza kwenye Lori
lililokuwa mbele yake ambalo halikuwa na mzingo kitendo kilichofanya paa
la basi hilo kukatwa wa juu ambapo watu 12 waliokuwa ndani ya basi
ndogo hilo kufariki dunia papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya .
Hata
hivyo alisema , majeruhiwa mmoja kati ya saba alifariki dunia wakati
alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro
alipofikishwa kutoka eneo la tukio na kutambuliwa na ndugu zake kuwa ni
Haji Mzaniwa ( 38), mwimbaji wa kikundi hicho. |
0 comments:
Post a Comment