Hapa walisimama pamoja na wanahabari hawapo pichani kuwaombea wasanii 12 wa Five Stars waliotangulia mbele ya haki. Na Ripota Wetu Jumanne,
Tarehe 22 Machi – Maandalizi kwa ajili ya onyesho la Tuzo za Muziki za
Kili yamekamilika ambapo waandaaji wa Tuzo hizo, Kampuni ya Bia Tanzania
TBL, kupitia kinywaji chake cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager
wametangaza wasanii watakaotoa burudani katika onyesho la utoaji wa Tuzo
hizo litakalofanyika Jumamosi ya Tarehe 26, Machi 2011 katika Ukumbi wa
Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, David Minja aliwaambia
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana ya kuwa Utoaji wa Tuzo za
mwaka huu utapambwa na burudani tofauti kutoka kwa wasanii mbalimbali na
kuogezea kuwa mwaka huu onyesho litakuwa katika mwonekano wa kisasa
zaidi kulinganisha na miaka ya nyuma.
“Tumekuwa tukidhamini Tuzo
hizi kwa miaka kadhaa sasa na kila mwaka tumekuwa tukionyesha staili
tofauti katika uboreshaji wa Tuzo hizi. Mwaka huu tumeziboresha zaidi na
nina uhakika wale watakaofika kushuhudia onyesho hili watakuwa
mashahidi,” Alisema Minja
Minja alisema kuwa wasanii wanaowania
tuzo hizo na wale watakaotoa burudani watakaribishwa katika ukumbi huo
kwa njia ya kipekee, na kuhojiwa na vyombo vya habari. “Tumeamua kutumia
wasanii wa ndani na tuna imani na wanachokifanya katika suala zima la
kutoa burudani,” Alisema Minja.
Alisema lengo la Tuzo hizi
zinazodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ni kufikisha muziki
wa Tanzania katika kilele cha mafanikio, na kuongezea kuwa mwaka huu
wameona ni vyema kuwapa nafasi kubwa wasanii wa hapa nyumbani kutoa
burudani kama sehemu ya kuwapa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika
sanaa ya muziki,” alisema Minja.
Wasanii watakaotumbuiza katika
utoaji wa Tuzo hizo ni Ali Kiba, THT, Banana Zoro, Linah, Diamond, Joe
Makini, C Pwaa, 20%, Mzee Yusuf pamoja na Mapacha Watatu na Stara
Thomas. Halikadhalika kutakuwa na burudani ya pamoja kutoka kwa washindi
wa Tuzo za Kili kwa mwaka jana.
Kwa mujibu wa Minja, Tiketi kwa
ajili ya onyesho hilo zimeshaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali jijini
Dar es Salaam kwa bei ya 25,000/- kwa tiketi za VIP na 15,000/- kwa
tiketi za kawaida.
Minja alisema kuwa watu watakaolipa kiingio
cha VIP watapata bia za Kilimanjaro Premium Lager bure, wakati kutakuwa
na bia mia moja za Kilimanjaro Premium Lager kwa watu mia moja wa kwanza
kuingia ukumbini.
Tuzo zinazoshindaniwa kwa mwaka 2010/ 2011 ni
Msanii wa kike bora wa Muziki, Msanii wa Kiume Bora wa Muziki, Mwibaji
bora wa Kike, Mwimbaji Bora wa Kiume, Wimbo Bora wa Taarab, Wimbo bora
wa Mwaka. Nyingine ni Wimbo bora wa Kiswahili (bendi), Wimbo bora
R&B, Wimbo bora wa Hip Hop, Wimbo bora wa Ragga, Rapa bora wa Mwaka
(Bendi), Msanii bora wa Hip Hop, Wimbo bora wa Africa Mashariki,
Mtayarishaji bora wa Muziki, Video bora ya muziki ya Mwaka na Msanii
mpya anayechipukia, Wimbo bora wa Kushirikishwa/ Kushirikisha, Wimbo
bora wa asili na Wimbo bora wa Rhumba. |
0 comments:
Post a Comment