MAPATO STARS v CAR
Mechi
ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika (CAN) zitakazochezwa Gabon- Equatorial Guinea mwakani kati ya
Taifa Stars na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) lililofanyika Machi 26
mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 110,552,000.
Watazamaji
21,117 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa kiingilio cha sh.
3,000, sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 40,000.
Asilimia
moja ya mapato hayo ambayo ni sh. 1,105,520 yatakabidhiwa kwa Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya waathirika wa mabomu ya Gongo
la Mboto.
UWAKALA WA WACHEZAJI
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limepanga mtihani wa uwakala wa
wachezaji kufanyika duniani kote Machi 31 mwaka huu. Mtihani huo uwa wa
sehemu mbili; maswali kutoka FIFA na kwa shirikisho la mpira wa miguu
kwa nchi husika.
Hadi
sasa hakuna Mtanzania aliyeomba kufanya mtihani huo, hivyo kuwa na sifa
ya kuwa wakala wa wachezaji anayetambuliwa na shirikisho hilo.
LIGI YA TAIFA 2010/2011
Ligi
ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa itachezwa Juni mwaka huu
ambapo katika hatua ya awali itakuwa na makundi manne. Makundi hayo
yatakuwa katika mikoa ya Pwani, Ruvuma, Kigoma na Singida.
Kundi
la Pwani litakuwa na mabingwa wa Pwani, Dar es Salaam- 1, Dar es
Salaam- 2, Tanga, Lindi na Mtwara. Ruvuma ni Mbeya, Iringa, Rukwa,
Morogoro, Dar es Salaam- 3 na Ruvuma. Kigoma ni Tabora, Kagera, Kigoma,
Shinyanga, Mara na Mwanza wakati Singida ni Arusha, Manyara, Singida,
Kilimanjaro, Dodoma na Shinyanga.
TIMU YA U23.
Timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 imewasili kwa ndege ya
Kenya Airways kutoka Cameroon kupitia Nairobi, Kenya. U23 ilikuwa huko
kwa ajili ya mechi za awali za Olimpiki ambapo Machi 27 ilicheza dhidi
ya wenyeji na kufungwa mabao 2-1.
Baada
ya kuwasili wachezaji watapewa mapumziko ya siku moja kabla ya kurejea
kambini kujiandaa kwa mechi ya marudiano itakayofanyika Aprili 9 mwaka
huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam |
0 comments:
Post a Comment