TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, February 24, 2011

Obama akashifu ghasia nchini Libya

3:18 PM
Rais Barrack Obama wa Marekani amekashifu machafuko yanayo endelea nchini Libya, katika hotuba yake ya kwanza kwenye runinga tangu mageuzi yaanze nchini Libya, yapata wiki moja sasa.

Amesema kuwa ukatili unaotumiwa na vyombo vya serikali kukabili waandamanaji haukubaliki kamwe na kuwa serikali yake inatathhmini hatua za kuchukua.
Japo hakutoa maelezo zaidi, alidokeza kuwa waziri wa mashauriano ya nje Hillary Clinton atasafiri mjini Geneva, Uswizi, kushauriana na nchi zingine.

Huku hayo yakiarifiwa maelfu ya waandamanaji wanaopinga serikali wamekuwa wakisherehekea kile wanachokiita ushindi mkubwa Mashariki mwa Libya.
Wakaazi mjini Tripoli wamesema wanaogopa kutoka nje kwa sababu wana wasiwasi wanajeshi wanaounga mkono serikali huenda wakawafyatulia risasi.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema yamethibitisha kuwa watu wasiopungua mia tatu wameuwawa tangu makabiliano hayo kuanza wiki iliyopita.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA