Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimfariji Mkurugenzi wa Baraza la
Manispaa Zanzibar Rashid Ali Juma (45) alipomtembelea leo katika
Hospitali ya Aga khan jijini Dar es salaam alikolazwa kwa matibabu
kutokana na kuumia vibaya sehemu za usoni, tumboni, kifuani na ubavuni
baada ya kumwagiwa Tindikali na Mtu asiyejulikana, wakati alipokuwa
amekaa nje ya Msikiti wa Amani mjini Zanzibar baada ya kumalizika kwa
Ibada ya Sala ya Insha saa 2:45 usuku, siku ya Alkhamis . Kwa muujibu wa
madaktari wanaomhudumia Mkurugenzi huyo, wamemuambia Makamu wa Rais
kuwa hali yake inaendelea Vizuri.
Picha na mdau Amour Nassor wa VPO.
Picha na mdau Amour Nassor wa VPO.
0 comments:
Post a Comment