Jacob
Nyajiego(mwenye suti nyeusi) akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya
majeneza yaliyohifadhi miili ya marehemu mke wake, Rozi Nyajiego(34) na
watoto wake wawili,Clementina Nyajiego(4)na Stella Nyajiego(miezi
3)waliokufa kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba wakati wa milipuko ya
mabomu.Ibada ya kuwaaga ilifanyika nyumbani kwake Mzambarauni,Gongo la
Mboto Dar es Salaam. Miili ya marehemu hao ilisafirishwa kwenda Rorya,
mkoani Mara kwa maziko.Picha na Fadhili Akida
Katibu Mkuu wa Chadema,Dk.Willibrod Slaa akiwa na Mke wake kwenye mazishi ya mama
na watoto wake wawili kutoka familia moja ya Jacob Nyajengo wa
Mzambarauni,waliokufa kwa kuangukiwa na nyumba ya jirani, kutokana
mabomu yaliyolipuka kutoka ghala la Silaha katika kambi ya Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gongo la Mboto,Dar es Salaam.Mheshimiwa Dk Wilbrod Slaa alifuatana pia na wabunge kadhaa kwa tiketi ya chama hicho.Picha hii na Mdau Bashir Nkromo


0 comments:
Post a Comment