TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, December 6, 2010

Soma Kisa Cha Raia Wa Kenya Aliyekuwa Na Wake 120, Aliyekufa Na Kuzikwa Desemba 5. 2010.

9:36 PM
Mwanaume wa nchini Kenya aliyejulikana kwa jina la Ancentus Akuku maarufu kwa jina la " Akuku Danger" ambaye huenda akawa mwanaume aliyeoa wanawake wengi kuliko wanaume wote duniani, ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 94 amefariki na kuzikwa jumapili ya tarehe 5 Desemba 2010

Katika maisha yake, Akuku alioa jumla ya wanawake 130 kati ya hao wake 30 aliwapa talaka.

Kama jina lake linavyobashiri "Danger", (hatari), Akuku alikuwa na watoto 210,ikiwa wa kiume ni 106 na wakike 104. Watoto wake wa kike 35 na wa kiume 20 wamefariki dunia.

Kwa mujibu wa mtoto wake mkubwa, Akuku alizimia akiwa kwenye mazingira ya nyumba yake mjini Kisumu, alipowahishwa hospitali alifariki dunia.

Akuku alimuoa mke wake wa kwanza Dinah Akuku, mwaka 1939, wakati mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 79, Akuku alifunga ndoa na msichana kigori mwenye umri wa miaka 18. Huyo ndiyo alikuwa mwanamke wa mwisho kufunga ndoa na Akuku.


Ukoo wa Akuku una shule mbili zilizojengwa na Akuku ili kuwapa elimu watoto na wajukuu zake na pia wanamiliki kanisa lao moja kwaajili ya ibada.

Dr Tom Akuku ambaye ni mtoto mkubwa kuliko wote wa kiume wa Akuku, alisema kuwa ingawa hati walizo nazo zinaonyesha Akuku ana watoto 210, huenda baba yao akawa na watoto zaidi ya 210.

"Mzee alikuwa na watoto wa kike 104 na wa kiume 106 hivyo kufanya jumla ya watoto 210, lakini naamini kutakuwa na watoto wengi hawamo kwenye listi".

"Idadi ya wajukuu ni zaidi ya 1,800", alimalizia kusema Dr. Akuku.

span>(Kipandulablog)


1 comments:

Anonymous said...

the storry z interesting@

Post a Comment

 
BONYA HAPA