Nakala ya kiingereza ya Kitabu cha Wasifu wa JK kama kinavyoonekana. Picha ya chini ni Profesa Nyang'oro akitia saini nakala za kitabu hicho zilizogaiwa bure kwa wageni wote waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo. Vitabu hivyo vitaanza kuuzwa kwenye duka la vitabu la Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kwa gharama ya shillingi 25,000/=
JK akiongea wakati wa uzinduzi wa kitabu chake
Mwandishi wa Kitabu cha Wasifu wa JK Profesa Julius Nyang'oro akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua kitabu hicho ambacho alikiandika na kuelezea sababu mojawapo iliyomfanya aandike kitabu hicho ni kutokuwa na kitabu cha aina hiyo kwa viongozi wetu wa nchi isipokuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
JK akizundua vitabu viwili (cha kiingereza na kiswahili) kwa wageni waliohudhuria hafla hiyo wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho akishuhudiwa na Mama Salma Kikwete na mwandishi wa kitabu hicho Profesa Nyang'oro
JK akionesha vitabu hivyo akiwa na mwandishi wake Profesa Nyang'oro
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba wakiongea na Profesa Nyang'oro ambaye ndiye mwandishi wa kitabu cha Wasifu wa JK wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Maendeleo ya Vijana Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Shukuru Kawambwa.
Baadhi ya wanafamilia ya Mheshimiwa Rais Kikwete na wageni waalikwa wakiperuzi kurasa za kitabu cha Wasifu wa JK
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Bwana Beno Malisa akizungumza na Miraji Kikwete kwenye uzinduzi wa Kitabu Cha Wasifu wa JK Ikulu jijini Dar es salaam.
1 comments:
Wasifu wake upo kwenye wikipedia. Ufisadi tu huu, yeye kama raisi ni nani asiyejua wasifu wake!
Post a Comment