TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, October 3, 2009

12:33 AM
Zimbabwe yashtakiwa kwa utesaji
Jestina Mukoko pamoja na wanaharakati wengine wanane wamemfungulia mashtaka kamishna mkuu wa polisi, waziri mmoja wa serikali na maafisa wengine wa serikali.

Mahakama kuu imemaua kutupilia mbali mashtaka yote yanayomkabili yakiwemo yale ya ugaidi, baada ya kubaini kuwa aliteswa akiwa rumande.

Mawakili wa Bi Mukoko, walidai kuwa alizamishwa majini, kufungiwa ndani ya jokofu na kisha kuchapwa.

Mukoko alituhumiwa kwa kuhusika na njama ya kupindua serikali ya rais Robert Mugabe, madai aliyoyakanusha vikali.

Kwa mujibu wa wakosoaji, madai hayo yalitolewa ili kuwafunga vinywa wapinzani wa Mugabe kutoikosoa serikali yake.

Wadadisi wanasema hatua ya kutupilia mbali mashtaka dhidi ya wanaharakati hao huenda ikapunguza hali ya wasiwasi katika seriakli ya muungano.

Waziri mkuu Morgan Tsvangirai alizungumzia swala hilo mapema mwaka huu akisema kuwa kesi iliyomkabili Mukoko ilihujumu serikali ya muungano ya Zimbabwe.

Wafadhili kwa sasa hawako tayari kuanza kutoa msaada kwa Zimbabwe, kwa sababu ya madai ya visa vya ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo.

Wengi wa waliokamatwa, walikuwa wafuasi wa Waziri mkuu Morgan Tsvangirai, ikiarifiwa kuwa maafisa wa shirika la ujajusi ndilo lilifanya mateso hayo.

Bi Mukoko aliachiliwa kwa dhamana tangu mwezi Mei mwaka jana ingawa alitoweka kutoka nyumbani kwake tangu Disemba hadi baada ya wiki tatu.

Serikali ilikana kumzuilia Mukoko ingawa baada ya mwezi mmoja alifikishwa mahakamani kujibu mashataka ya ugaidi.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA