TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, October 3, 2009

Mabasi yamiminika kuwekewa mikanda

12:41 AM
Wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani wamejitokeza kwa wingi kupeleka mabasi kuwekewa mikanda katika viti vya abiria kusaidia kupunguza ajali zinazotokea barabarani mara kwa mara nchini.

Hatua hiyo imetokana na agizo lililotolewa na Jeshi la Polisi nchini kuwataka wamiliki wa mabasi ya mikoani kuweka mikanda katika viti vya abiria ambapo mwisho ilikuwa ni jana.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, James Kombe, alisema madereva wanazidi kujitokeza kwa wingi kupeleka magari yao kutekeleza agizo hilo.

Kamanda Kombe alisema mabasi yote ambayo hayatakuwa yamewekewa mikanda baada ya kumalizika kwa Wiki ya Usalama Barabarani, yatachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kamanda Kombe alitoa agizo hilo Agosti, mwaka huu ikiwa ni hatua za kukabiliana na ongezeko la ajali za barabarani nchini.



0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA