TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, October 3, 2009

Polisi wakwamisha kesi ya anayedaiwa kumkashifu Mkapa

12:32 AM
Kesi inayomkabili raia wa Iraq, Anney Anney (58) ya kuwakashifu marais wa awamu ya pili na ya tatu na kutoa maneno ya uchochezi, imeahirishwa kwa mara nyingine baada ya upande wa mashitaka kudai hauna jalada la polisi.

Kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya kusikilizwa iliahirishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam na Hakimu Samwel Maweda.

Mshtakiwa huyo ambaye ana ulemavu wa mguu, alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Julai 27, mwaka huu.

Mshtakiwa alidaiwa kutoa maneno ya uchochezi kwa marais, Alhaj Ali Hassan Mwingine na Benjamin Mkapa katika eneo la Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mshtakiwa anadaiwa kuwatuhumu viongozi hao kuwa walikuwa wanaendesha nchi kwa maslahi yao binafsi bila kuwajali wananchi.

Upande wa mashtaka ulidai Julai 23 mwaka huu, saa 9;00 mchana katika eneo la Ikulu jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alitoa maneno ya uchochezi kupitia mabango aliyokuwa ameshika kuwa Mwinyi aliua Azimio la Arusha na Mkapa aliuza mashirika ya umma na ardhi kwa Wazungu na Waarabu na utu wa utaifa wa Watanzania.

Mshtakiwa alikana mashtaka na kupelekwa rumande kwa kukosa dhamana.



0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA