TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, October 7, 2009

Samaki waua mtu Jijini Dar

10:11 PM

Samaki katika Bahari ya Hindi Jijini Dar wanadhaniwa kumtafuna mtu mmoja hadi kumuua na mwili wake kuokotwa jana ukiwa ufukweni pale katika eneo la Kurasini Jijini.

Mtu huyo aliyeuawa kwa kuliwa na samaki, ametambuliwa kwa jina la Nsajigwa Malonge, 35, mkazi wa Vijibweni, Kigamboni Jijini.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Liberatus Sabas, amesema mwili wa marehemu huyo uliopolewa kandoni mwa bahari jana, mishale ya saa 12:00 asubuhi, katika ufukwe wa Kitopeni, Kurasini Jijini Dar.

Akasema mwili wa marehemu huyo umekutwa ukiwa na majeraha tele yanayodhaniwa kuwa ni matokeo ya kuliwa na samaki wasiofahamika ni wa aina gani, ndani ya Bahari ya Hindi.

Akielezea zaidi tukio hilo, Kamanda Sabas amesema kuwa awali, mtu huyo alionekana Oktoba 4 mwaka huu, katika ufukwe wa Kitopeni, akiwa ameongozana na baba yake aitwaye Benald Ambilikile.

Akasema kuwa marehemu alionekana akiwa amelewa chakari kutokana na kunywa pombe kwa wingi.

Akasema marehemu na baba yake, walipanda mtumbwi wakielekea Kigamboni.

Hata hivyo, akasema walipofika ufukweni, marehemu hakuonekana hadi jana wakati mwili wake ulipokutwa ukielea katika ufukwe huo, eneo la Kurasini.

Akasema majeraha mengi katika mwili wa mtu huyo yamekutwa sehemu za mgongoni, ambako pia kulikuwa na mapovu yanayoashiria kuwa ameshambuliwa na samaki.

Hata hivyo, Kamanda Sabas amesema uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo unaendelea na hadi sasa, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Temeke.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA