
Utafiti uliofanywa na BBC umegundua kwamba makabila yanayopingana nchini Kenya ambayo yalipigana baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 yanakusanya silaha.
Makabila hayo yanajiandaa iwapo ghasia zitaibuka katika uchaguzi wa mwaka 2012.
Inahofiwa kwamba wanakijiji katika mkoa wa Rift Valley wameamua kuacha kutumia silaha za asili kama pinde na mishale na badala yake kutumia bunduki.
Maafisa wa serikali wamesisitiza kwamba wanapambana na ongezeko kubwa la silaha zinazoingia kinyume cha sheria.
Hata hivyo wamekuwa wakikosolewa vikali kwa kushindwa kuwaadhibu viongozi wa ghasia hizo baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Vurugu hizo zilisababisha vifo vya takriban watu 1,300.
Serikali ya muungano iliundwa mwanzoni wa mwaka 2008 kwa nia ya kutuliza vurugu hizo.
0 comments:
Post a Comment