TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, October 1, 2009

PINDA;MSIFAE SHUTI

4:40 PM

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amenukuliwa akisema watanzania waache kuvaa suti kwani ni gharama kwa wananchi maskini. Bofya hapa.

Kwa nchi yenye matatizo mengi ya msingi kama Tanzania, nadhani Waziri Mkuu hakuwa sahihi kusema maneno haya. Suala la kuvaa suti ni la mtu binafsi kutegemea na kipato na uwezo wake. Suala la suti halina uhusiano na mapato wala uchumi wa nchi.

Kuna mambo mengi ya msingi kama vile ongezeko la umaskini nchini, Kilimo Kwanza, elimu na miuondombinu duni na matumizi yasiyo ya lazima katika Serikali , kwa mfano ununuzi wa magari ya fahari. Waziri Mkuu angeelekeza nguvu katika masuala haya na sio uvaaji wa suti.

Waswahili husema , uungwana ni vitendo. Yafaa Waziri Mkuu aongoze kwa vitendo. Inabidi yeye aongoze kuacha uvaaji suti ili wengine wafuate.
Uvaaji wa sasa wa Waziri Mkuu hauendani na anachokisema. Isije ikawa kauli zake zinamaanisha, fanyeni kama ninavyosema, na si ninachokifanya.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA