TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, October 1, 2009

CUF watikisa Dar

4:43 PM

Maelfu ya wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) wakiongozwa na viongozi wao wa kitaifa, jana walilitikisa jiji la Dar es Salaam kwa kufanya maandamano ya amani yaliyolenga kuwasilisha madai yao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ya kutaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ivunjwe.

CUF inadai kwamba NEC imeshindwa kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki nchini tangu iundwe miaka 17 iliyopita na kwa hiyo, inataka ivunjwe na pia, Mwenyekiti wake, Jaji Lewis Makame ajiuzulu.

Maandamano hayo yaliyopokelewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, katika viwanja vya Kidongo Chekundu, yalianza saa 5:10 asubuhi, eneo la Sheli, Buguruni, baada ya Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akiwaongoza viongozi wengine wa kitaifa kufika katika eneo hilo.

Viongozi wengine walioshiriki maandamano hayo ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Juma Duni Haji, Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma, Salim Bimani, Naibu wake, Ashura Mustapha na Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa Chama hicho, Shaweji Mketo.

Maandamano hayo yalipita katika Barabara ya Uhuru na Bibi Titi Mohamed huku yakisindikizwa na magari ya polisi aina ya Lond Rover Defender na kupokelewa na Tendwa katika viwanja vya Kidongo Chekundu, saa 6:30 mchana.

Wakati wote wa maandamano, waandamanaji walisikika wakiimba nyimbo mbalimbali za kuikejeli serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na NEC, huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe unaoshinikiza NEC ivunjwe na kuundwa tume mpya huru.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA