TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, October 9, 2009

10:16 AM

Mstaafu Afrika Mashariki Dar agongwa na gari, kufa


Mstaafu mmoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliyekuwa akifanya kazi katika Mamlaka ya Bandari, Bw. Hilary Mapunda, 81, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akijaribu kuvuka barabara.

Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Akili Mpwapwa, amesema tukio hilo limetokea mishale ya saa 3:45 asubuhi, katika barabara ya Nyerere eneo la Vingunguti Jijini Dar es Salaam.

Akasema kuwa mstaafu huyo, mkazi wa Vingunguti Karakana, aligongwa na gari lisilofahamika ambalo lilikuwa likitokea eneo la Uwanja wa Ndege, kuelekea TAZARA.

Akasema mstaafu huyo alifariki dunia wakati akiwa njiani ili kuwahishwa katika Hospitali ya Amana kwa ajili ya matibabu.

Kamanda huyo akasema polisi wanaendelea uchunguzi kulibaini gari lililosababisha ajali na kwamba mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Amana.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA