TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, October 24, 2009

Bwenyenye wa Kenya aachiliwa

9:19 AM

Mkenya mwenye asili ya kizungu aliyehukumiwa kifungo cha miezi minane kwa kumuua kwa kutokusudia mwindaji haramu katika shamba lake ameachiliwa huru baada ya kuwa ndani kwa miezi mitano.

Thomas Cholmondeley alihukumiwa kufungwa mwezi mei kwa kumpiga risasi na kumuua Robert Njoya mwaka 2006, na hii ni baada ya kuwa ndani kwa miaka mitatu akisubiri hukumu yake.

Aliachiliwa kutokana na kuonyesha tabia nzuri na kwa kuwa alikuwa na chini ya miezi sita kumaliza kifungo chake,maaafisa wa magereza walisema.

Wakati wa hukumu,hakimu alipunguza kosa la mauaji na kuwa kuuwa bila kukusudia.

Hakimu alisema Cholmondeley hakuonyesha "nia mbaya".

Cholmondeley, mwenye umri wa miaka 40 alipata elimu yake katika chuo cha Eton uingereza,alimpiga risasi bwana Njoya aliyekuwa akiwinda katika shamba lake la ekari 55,000 huko Soysambu karibu na ziwa Naivasha nchini Kenya.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA