Kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 200, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Armatus Liyumba,
imeendelea tena leo ambapo shahidi wa pili katika shauri hilo ametoa ushahidi wake.
Kesi hiyo inasikilizwa na mahakimu watatu ambao ni Edson Kasimwongo, Lameck Mlacha na Benedict Mwinga katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Shahidi huyo ni Meneja wa Masuala ya Bodi wa Benki Kuu (BoT), Justo Tongola ,45,
Akiongozwa na wakili wa Serikali, Juma Ramadhani, Tongola amesema miongoni mwa kazi zake ni kuandaa mikutano ya bodi ambapo huhakikisha wajumbe wanapata taarifa, makabrasha ya mikutano na kuweka kumbukumbu.
Akaieleza mahakama hiyo kuwa kisheria bodi ya BoT, ndiyo yenye mamlaka ya kutengeneza sera na kupitisha bajeti.
Hata hivyo akasema gavana ndiye mwenye mamlaka ya mwisho kwenye kutoa maamuzi.
Upande wa mashtaka unatarajiwa kuleta mashahidi kumi, miongoni mwao wakiwa ni Professa Joseph Semboja, Professa Letice Rutashobya, Professa John Nduguru, Michael Shirima, Bosco Kimela, Seif Mohamed na Jafari Uledi.
Katika shauri hilo, Liyumba anatuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 221, kupitia kwenye mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo.
0 comments:
Post a Comment