TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, October 24, 2009

9:18 AM

Dar kukosa maji leo


Wakati mgawo wa umeme unaendelea kulitikisa taifa, kesho wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, watakumbwa na balaa lingine.

Balaa lenyewe linafuatia tangazo la Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) kuwa hakutakuwa na maji kwa siku nzima.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari inasema kuwa, mitambo yake miwili ya kuzalisha maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu, itazimwa kwa saa 12 kesho.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mitambo hiyo itazimwa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 2:00 usiku na kwamba sababu za kuzimwa kwa mtambo huo ni matengenezo ya vifaa vya umeme katika pampu za kusukumia maji.

Taarifa hiyo imesema kuzimwa kwa mitambo hiyo kutasababisha maeneo mbalimbali ya Jiji kukosa maji.

Maeneo hayo ni pamoja na Tegeta, Boko, Bunju, Mbezi Beach, Kawe, Mikocheni, Masaki, Oysterbay, Msasani Mlalakuwa, kijitonyama na Sinza.

Maeneo mengine ni Magomeni, Ubungo eneo la viwanda, Manzese, Mwenge, Mwananyamala, Kinondoni, ilala, baadhi ya maeneo ya Chang’ombe, Keko, Upanga, Magogoni na maeneo ya katikati ya Jiji.

Mengine ni pamoja na yale yanayopata maji kutoka mtambo wa Ruvu Juu ambayo ni Mlandizi, Kibaha Kibamba, Mbezi Juu, Kimara, Ubungo, Tabata na baadhi ya maeneo ya Manzese na Mabibo.

Mamlaka hiyo imesema huduma ya maji inatarajiwa kurejea katika hali yake ya kawaida Jumapili jioni.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA