TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, October 30, 2009

7:52 AM

Babu Seya, wanawe wahaha kujinasua


Mwanamuziki Nguza Viking almaarufu kama Babu Seya pamoja na wanawe Papii Kocha, Nguza Mbangu na Francis Nguza, wameanza harakati za kujinasua na kifungo chao cha maisha walichopewa na Mahakama Kuu baada ya kukutwa na hatia katika shtaka kubaka.

Taarifa ambazo Alasiri imezinyaka toka kwenye chanzo kimoja cha uhakika, zinadai kuwa Nguza na wanawe hao wameshawasilisha nyaraka muhimu pale kwenye Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, nia ikiwa ni kutaka majaji wa mahakama hiyo ya juu nchini kubatilisha uamuzi uliowatia hatiani.

Awali, Nguza na wanawe hao walihukumiwa kifungo cha maisha na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kisha baadaye na Mahakama Kuu.

Wote wanne, walikutwa na hatia ya kuwabaka watoto kumi wa Shule ya Msingi Mashujaa iliyopo pale Sinza Jijini Dar.

Chanzo hicho cha uhakika kimedai kuwa Nguza na wanawe wameshapeleka rufaa yao kwenye Mahakama ya Rufaa tangu wiki iliyopita.

Hata hivyo, tarehe na siku ya kuanza kusikilizwa kwa rufaa hiyo kutategemea maamuzi ya Mahakama yenyewe ya Rufaa.

Awali, mwaka 2004, Nguza na wanawe walikutwa na hatia hiyo na kuhukumiwa kifungo cha maisha na Hakimu Addy Lyamuya, ambaye wakati huo alikuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hata hivyo, wote hawakuridhishwa na uamuzi huo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kukata rufaa ya kupinga hukumu katika Mahakama Kuu.

Hata hivyo, baada ya kesi yao kupitiwa upya na Mahakama Kuu, Jaji Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao na hivyo hukumu ya kifungo cha maisha ikabaki palepale.

Katika harakati zote hizo, Nguza na wanawe wamekuwa wakitetewa na Wakili Herbert Nyange, ambaye amekuwa akidai kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani wateja wake..

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA