
Waziri mkuu wa Denmark, Lars Loekke Rasmussen, na ambaye nchi yake itakuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa Copenhagen kuzungumzia hali ya hewa ulimwenguni mwezi Desemba, amesema haamini mataifa yataafikiana wakati huo na kupunguza gesi zinazoongeza joto ulimwenguni.
Kiongozi huyo ametamka hayo huku viongozi wa Ulaya wa EU wakijiandaa kwa mkutano mjini Brussels kuzungumzia ni vipi nchi zao zitaweza kuyasaidia mataifa yanayoendelea kupunguza gesi zinazoongeza joto ulimwenguni.
Hata hivyo mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amewaelezea waandishi kwamba mkutano huo wa mwezi Desemba huenda bado ukapata ufanisi.
Amesema hata ikiwa makubaliano hayatatiwa saini moja kwa moja, yanaweza kupitishwa baadaye.
0 comments:
Post a Comment