TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, September 28, 2009

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

7:52 PM
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ambaye wizara yake inahusika moja kwa moja katika kuhakikisha kuwa inasimamia kwa ukaribu sakata la kampuni tata ya kuzalisha umeme ya Richmond Development.

MZIMU wa Kampuni ya Richmond Development (LLC), uliowekwa kiporo katika kikao cha Bunge kilichopita, unatarajiwa kuibuka tena kabla ya kikao kijacho cha Bunge, baada ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, kujipanga kujadili taarifa ya utekelezaji wa maazimio yake kutoka serikalini.

Katika Mkutano wa Bunge uliomalizika mwishoni mwa mwezi Agosti, Bunge liliitaka serikali ipitie na itekeleze maazimio yote ifikapo Bunge la mwezi Novemba, ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha maafisa wake waandamizi, walioshiriki kwenye mkataba huo wa kifisadi uliosaniwa Juni 23, 2006.

Tayari ratiba ya vikao vya Kamati za Bunge ambayo gazeti hili imefanikiwa kupata nakala yake, inaonyesha bayana kwamba, utekelezaji wa maazimio ya Richmond ni moja ya ajenda ambayo itafikishwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ili kujadiliwa.



0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA