
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Bernard Kouchner, amesema yeye na mwenzake wa Poland wamemuandikia waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, kuhusu kukamatwa kwa muongozaji wa filamu , Roman Polanski.
Akizungumza katika radio ya Ufaransa Bwana Kouchner amekielezea kitendo cha kukatwa kwa Polanski kama ni ukatili. Bwana Polanski ambaye ana uraia wa Ufaransa na Poland alitiwa nguvuni siku ya jumamosi nchini Switzerland.
Vyombo vya sheria mjini Los Angeles wanataka bwana Polanski arejeshwe Marekani ili ahukumiwe kwa kufanya ngono na binti wa miaka 13 hapo mwaka 1977.
0 comments:
Post a Comment