TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, September 28, 2009

Madai ya kumpindua Mugabe yaondolewa

7:59 PM

Mwanaharakati huyo, Jestina Mukoko, alilia na kuwakumbatia marafiki zake kufuatia uamuzi wa mahakama ya juu zaidi ya kutupilia mbali madai kwamba pamoja na washukiwa wengine wanane walipanga njama ya kuipindua serikali ya Rais Robert Mugabe.

"Sikuamini madai kama hayo yanaweza kutolewa dhidi yangu," alisema.

Bi Mukoko aliiambia mahakama hiyo kwamba aliteswa na maafisa wa usalama walipomkamata akiwa nyumbani kwake.

Jaji Mkuu Godfrey Chidyausiku alitupilia mbali kesi hiyo na kukubaliana na mawakili wa Bi Mukoko kwamba maafisa wa usalama walikiuka haki zake.

Watu watatu wangali wanakabiliwa na mashtaka hayo ya kutaka kuipindua serikali ya Rais Mugabe.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA