TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, September 8, 2009

Watatu hatiani njama za kuripua ndege

9:08 PM

Watu watatu wamepatikana na hatia ya kula njama ya kuua maelfu ya watu kwa kulipua ndege za kutoka London hadi Marekani kwa mabomu ya kienyeji yaliyochanganywa vimiminiko.

Mahakama ya Woolwich Crown imemtia hatiani Abdulla Ahmed Ali, mwenye umri wa miaka 28, Tanvir Hussain, wa umri wa miaka 28, and Assad Sarwar, 29, kwa kula njama za kulipua mabomu yaliyobadilishwa yaonekane kuwa vinywaji.

Watu wengine wanne hawakukutwa na hatia ya kushiriki katika njama hizo za mpango wa mabomu ya kujitoa muhanga.

Watu hao watatu walikamatwa mwezi Agosti mwaka 2006 hatua iliyosababisha kuwekwe sheria mpya za kuingia na vinywaji au vitu vya majimaji hali iliyosababisha kero kwa wasafiri.

Mahakama ilielezwa wakati watu hao wakikamatwa, kiongozi wa njama hizo Ahmed Ali alikuwa na orodha ya ndege saba za Marekani na Canada zilizokuwa zilipuliwe katikati ya bahari ya Atlantic katika kipindi cha saa mbili na nusu.

Zilikuwa ni ndege zilizokuwa zisafiri kutoka uwanja wa ndege wa Heathrow London kuelekea San Francisco, Washington, New York, Chicago, Toronto na Montreal.

Msaidizi wake wa karibu, Sarwar, alikuwa ndie mwenye jukumu la kutafuta nyenzo za kutengenezea mabomu nyumbani kwake High Wycombe, Buckinghamshire, na nyumba iliyopo eneo la Walthamstow mashariki mwa London ndio ilikuwa kiwanda cha kutengenezea mabomu hayo.

Watu hao watatu kwa pamoja walichanganya dawa walizokusanya ambazo walipanga wasafiri nazo ndegeni zikiwa zinaonekana sawa na chupa za kawaida za vinywaji katika mabegi yao ya mikononi.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA