TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, September 11, 2009

1:13 PM

Walimu mbaroni kwa upotevu wa mtihani wa darasa la saba


Walimu watatu wa shule ya msingi pamoja na askari mgambo mmoja, wametiwa mbaroni mkoani Singida kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa mtihani wa taifa wa darasa la saba.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Celina Kaluba, alisema tukio hilo lilitokea Septemba 9, mwaka huu saa 8:00 mchana.

Kamanda Kaluba alifafanua kuwa mtihani uliopotea ni wa somo la Kiswahili.

Aliwataja walimu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za upotevu wa mtihani huo kuwa ni pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kisiluda ambaye ndiye aliyekabidhiwa mtihani huo uliokuwa ufanyike kwenye Shule ya Msingi Lainichungu, iliyopo tarafa ya Ihanja, Juma Mukiya (59).

Wengine kwa mujibu wa Kamanda Kaluba ni walimu wasaidizi Christopher Shaaban (47) wa Shule ya Msingi Mnang’ana, Kassim Kidimwa (32) wa Shule ya Msingi Msimihi na askari mgambo Jumanne Nangwa (38).

Alisema siku ya tukio, watuhumiwa hao kwa pamoja walihusika na upotevu wa mtihani huo uliokuwa ufanyike muda mfupi kabla ya kupotea katika shule hiyo ya msingi.

Kamanda Kaluba alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakati wanafunzi wakiwa darasani wakisubiri kuanza mtihani huo, ndipo mwalimu Mkiya alipofika darasani na kuanza kufungua makabrasha na kudai kuwa mtihani wa somo la Kiswahili hauonekani.

Alisema hali hiyo ilileta hofu kwamba mtihani huo umevuja na hivyo kumtafuta Afisa Elimu wa Mkoa.

Alisema Afisa Elimu wa Mkoa, alifanya juhudi za kupata mtihani mwingine na wanafunzi wakaendelea kufanya.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA