
Tsunami iliyoibuliwa kutokana na tetemeko kubwa la ardhi katika bahari ya Pacific Kusini, hadi sasa imekwishaua watu zaidi ya 100 katika visiwa vya Samoa.
Takriban watu 77 imearifiwa wamekufa katika kisiwa cha Samoa, zaidi ya 25 katika kisiwa cha American Samoa na takriban watu sita wamepoteza maisha katika kisiwa cha Tonga.
Wakaazi wa maeneo hayo pamoja na watalii iliwalazimu kukimbilia maeneo ya juu baada ya vijiji kuangamizwa kabisa. Mashua zilisombwa na maji hadi nchi kavu, huku magari na watu wakichukuliwa na maji hadi baharini.
Tetemeko lenye ukubwa wa 8.3 kiwango cha vipimo vya matetemeko, lilipiga siku ya Jumanne jioni na kuibua mawimbi ya bahari hadi urefu wa futi 15 katika baadhi ya sehemu za visiwa hivyo.
Visiwa vya Samoa kwa ujumla vina watu wanaofikia 250,000.
0 comments:
Post a Comment