TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, September 30, 2009

Mkuu wa tume ya ufisadi Kenya ajiuzulu

9:37 PM

Mkuu wa tume ya kupambana na rushwa nchini Kenya ambaye uteuzi wake ulikuwa umepingwa na watu wengi wa nchi hiyo, hatimaye amejiuzulu ikiwa ni wiki chache baada ya kuteuliwa na rais.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza la Reuters, Aaron Ringera amesema anajiuzulu kwa manufaa ya nchi.

Rais Mwai Kibaki alikuwa anataka jaji huyo mstaafu kutumikia muhula wa pili akiwa mkuu wa tume ya kupambana na rushwa nchini humo maarufu Kenyan Anti-Corruption Commission.

Lakini mapema mwezi wa Septemba, Wabunge walisema uteuzi huo wa rais ni kinyume na sheria na waliukataa uteuzi huo.

Waandishi wa habari wanasema Bwana Ringera alikuwa akilaumiwa na Wakenya kwa kutofanya vya kutosha katika kupambana na rushwa.

Alikuwa akipokea mshahara mkubwa akiwa mtumishi wa serikali, wa shilingi za Kenya milioni 2.5 kwa mwezi, kuliko mshahara anaopata rais.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA