TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, September 27, 2009

11:15 AM

TBS sasa kukagua bidhaa nje kabla ya kuja Tanzania


Shirika la Viwango Tanzania (TBS), linatarajia kuanza kukagua bidhaa mbalimbali katika nchi zinakotengenezwa ili kuona kama zina viwango kabla hazijaruhusiwa kuingia nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa TBS, Charles Ekelege, wakati akizungumza na Rais wa Shirika la Viwango Duniani (ISO), Dk. Alan Morrison.

Ekelege alisema mpango huo unaotarajia kuanza mwishoni mwa mwaka huu utasaidia kudhibiti bidhaa feki zinazoingizwa hapa nchini.

Alimwambia Dk. Morrison kwamba licha ya TBS kuendesha mipango mbalimbali ya udhibiti wa ubora lakini pia inaendesha mafunzo ya usimamizi wa ubora katika viwanda mbalimbali hapa nchini.

Alisema TBS ina idara saba ambazo zimejaa watalaamu wa fani mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa halisi zenye nembo yao.

Aliongeza kuwa ili kupambana na bidhaa feki, TBS imetoa vyeti vya ithibati kwa maabara nne kwa ajili kuendesha shughuli za kupima bidhaa.

Ili kutekeleza mkakati wa serikali wa kufikia malengo ya Maendeleo ya Milenia hadi kufikia mwaka 2015, Dk. Ekelege alisema TBS imejipanga ili kuhakikisha inatambuliwa kitafia na kimataifa kama kitovu cha shughuli za viwango na uhakiki wa ubora.

Kwa upande wake, Rais wa ISO, Dk. Morrison aliipongeza TBS kutokana na juhudi zake na kuahidi kuendelea kushirikiana nayo katika shughuli mbalimbali.

Alisema TBS imefanya kazi kubwa katika kusukuma mbele maendeleo ya nchi kwa kuhakikisha soko la Tanzania linakuwa na bidhaa zenye ubora badala ya kuwa feki.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA