TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, September 27, 2009

Mtoto asimulia bomu lilivyomuua mdogo wake Mbagala Dar

11:13 AM
Na Geofrey Nyang’oro

“NILIMKUTA mdogo wangu akiwa bado anahema, lakini sikutambua kama alikuwa na majeraha mengine hadi mama alipomuona na kuanza kulia.”

Ni kauli ya Hamza Athumani (15), mtoto aliyekuwa shuhuda wa kwanza kwenye tukio la mlipuko wa bomu la Septemba 24, lililosababisha vifo vya watoto watatu na wengine wanne kujeruhiwa vibaya.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili katika mahojiano maalumu, mtoto huyo anasema, “Nikiwa ndani nilisikia mlio mkubwa na kutoka nje kwenda kuangalia kuna nini."

Anasema mara baada ya kutoka, aliwakuta watoto wawili wakilia huku wakiwa wamejeruhiwa na bomu hilo, lakini alipoangalia mbele, aliona watoto wawili akiwemo mdogo wake ambaye kwa sasa ni marehemu wakiwa wameanguka chini na kulaliana.

“Nilipoangalia mbele niliona watoto wawili (marehemu Regina Chawala na marehemu Rajabu Saidi), walikuwa wameanguka huku Regina akiwa amemuangukia mdogo wangu,”anasema.

Anasema mara baada ya kuona hali hiyo alikwenda moja kwa moja eneo hilo na alipofika alikuta marehemu Regina akiwa hahemi kabisa, lakini mdogo wake aliyekuwa amelaliwa chini alikuwa anaonyesha dalili za kutaka kuzungumza lakini akawa hawezi.

Anasema kitendo hicho kilimfanya afanye kazi ya ziada ya kumuondoa na kumweka pembeni marehemu Regina Chawala na kisha kumchukua mdogo wake na kumbeba huku akiomba msaada kutoka kwa baba yake.

Anasema wakati anamchukua mtoto huyo, alichokuwa ameona yeye ni kutokea kwa jeraha sehemu za jicho jeraha ambalo lisababisha jicho hilo kutoka nje.

''Nilichoona mimi kwa mara ya kwanza ni jicho la mdogo wangu likiwa nje, lakini baadaye mama aligundua jereha jingine kubwa zaidi tumboni, jeraha ambalo lisabaisha utumbo wa mdogo wangu kutoka nje,”alisema Rajabu.

Rajabu anasema mara baada ya kufika kwenye uwanja wa nyumba yao, akiwa amembeba mdogo wake huku akiomba msaada kutoka kwa baba yake, mama mzazi alitoka nje na kuanza kulia.

Anasema kitendo cha mama yake kuanza kulia, kulimfanya aone jeraha hilo la tumboni na ndipo alipopoteza nguvu na kuanguka chini huku akiwa amembeba mdogo wake.

Anasema mara baada ya kuanguka chini alichukuliwa na watu na kuwekwa pembeni na kwamba alichoshuhuda ni umati wa watu kufika na kuzunguka eneo hilo.

``Nilisikia sauti ya watu ikisema leteni nguo tufunike mwili wa marehemu, lakini kwa wakati wote huo sikuona tena mwili wa mdogo wangu kwani watu walijaa na kuupakia kwenye gari kwa ajili ya kumkimbiza Hosptalini."



0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA