.jpg)
Wakati kazi ya uendelezaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura katika Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiendelea, vitendo vya hujuma sasa vimehamia kwenye mifugo ambapo kuku zaidi ya 100 wa Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa Kaskazini Pemba wameteketezwa kwa moto.
Katibu Mwenezi huyo, Kombo Hamad Yussuf, mkazi wa Kijiji cha Kangagani katika Jimbo la Ole Wilaya ya Wete, alikumbwa na kadhia hiyo usiku wa manane juzi ambapo alijulishwa na majirani zake kuwa banda lake la kuku lililopo nje kidogo ya kijiji anachoishi kuchomwa moto na kuku wote kuteketea.
0 comments:
Post a Comment