.jpg)
Uhai wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umeendelea kuwa mashakani baada ya Menejimenti ya kampuni hiyo kutoa notisi ya siku 60 kuanzia Septemba 10, mwaka huu na kutishia kuondoka iwapo muafaka baina ya Serikali na Rites hautafikiwa.
Kwa mujibu wa notisi hiyo, hadi Novemba 9, 2009 iwapo hakutakuwa na muafaka baina ya Serikali na Rites, menejimenti ya TRL itafungasha virago.
TRL inaendeshwa na menejimenti kutoka India ambayo imeajiriwa na kampuni ya Rites inayomiliki asilimia 51 ya hisa ndani ya kampuni ya TRL wakati Serikali ina hisa 49.
0 comments:
Post a Comment