TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, September 10, 2009

8:01 AM

Kesi ya vigogo wa DECI yapigwa tena kalend


Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, imeiahrisha kesi inayowakabili viongozi wa Taasisi ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) hadi Oktoba 12 mwaka huu kutokana na upelelezi wake kutokamilika.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mchungaji Jackson Mtaresi, Dominic Kigendi, Timothy Ole Loiting’inye, Samwel Mtaresi na Arbogast Kipilimba.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali, Justuce Mulokozi, ndio ulioiomba mahakama kuihirisha kwa kuwa upelelezi wake haujakamilika.

Ombi lilikubaliwa na mahakama chini ya Hakimu Mkazi Warialwande Lema anayeisikiliza kesi hiyo.

Viongozi hao wanashtakiwa kwa kuendesha na kusimamia mchezo wa upatu wa kuchangisha fedha kwa ahadi ya malipo maradufu, ulioitwa Panda Mbegu.

Wanadaiwa kufanya kosa hilo kwenye makao makuu ya DECI yaliyo katika eneo la Mabibo Mwisho wilayani Kinondoni.

Wanadaiwa kufanya kosa hilo kwa tarehe tofauti kati ya mwaka 2007 na Machi mwaka huu, ikiwa ni kinyume cha kifungu namba 171A (1) na cha (3) cha Kanuni ya Adhabu cha mwaka 2002.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA