.jpg)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Iddi kitaifa ambalo mwaka huu litafanyikia Jijini Dar.
Akizungumza na waandishi wa habari, Sheikh wa Baraza Kuu la Waislam nchini (BAKWATA), MKoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum amesema Baraza hilo litafanyika jioni ya saa 10:15, katika ukumbi wa Karimjee.
Aidha, Sheikh Salum amesema vilevile kuwa Swala ya Iddi ambayo itategemea muandamo wa mwezi, itafanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar na Mgeni Rasmi atakuwa Mufti wa Tanzania, Sheikh Shaaban Bin Simba.
Sheikh Salum amesema BAKWATA imewapa heshima kubwa Waislamu wa Jiji la Dar kwa ajili ya shughuli zote mbili, kwa matumaini kuwa wataitumia fursa hiyo kuimarisha umoja wao na kusameheana kwa utukufu wa kumalizika kwa mwezi wa Ramadhani.
Akasema ni matarajio ya BAKWATA kuwa waumini wengi watahudhuria, wakiwemo maimamu wa misikiti mbalimbali na pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali, hasa zile za Kiislamu.
''Baraza limetupa nafasi ya upendeleo kwetu sisi tuishio Jijini Dar ... ni muda mrefu sana tangu swala ya Idd El Fitri kufanyika kwetu kitaifa. Ni wajibu wetu kuitumia vyema fursa hii,'' akasema Sheikh Salum.
0 comments:
Post a Comment