TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, September 23, 2009

Hukumu kwa wauaji albino Kahama leo

5:32 PM

Mahakama Kuu Maaluum mjini Kahama mkoani Shinyanga, leo inatarajia kutoa hukumu kwa washtakiwa watatu katika kesi namba 24 ya 2009 ya mauaji ya mtoto albino, Matatizo Dunia (13).

Hukumu hiyo inayotarajiwa kuanza kusomwa saa 3:00 asubuhi, itatolewa na Jaji Gabriel Rwakibalila na baadaye kuendelea kusikiliza kesi nyingine za mauaji ya kukusudia ya albino na vikongwe namba 25 na 26.

Kutolewa kwa hukumu hiyo, kunafuatia pande zote mbili za mashitaka na utetezi, kukamilisha kutoa ushahidi na kufunga majumuisho ya mashitaka na utetezi wa upande wa washtakiwa hao.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Masumbuko Madata mkazi wa Ituga, Emmanuel Masangwa, mkazi wa Bunyihuna na Charles Kalamuji au Masangwa, mkazi wa kijiji cha Nanda wilayani Bukombe.

Wote wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya kukusudia yaliyotokea Desemba Mosi, mwaka jana katika kijiji cha Bunyihuna, Kata ya Iponya, Ttarafa ya Masumbwe wilayani Bukombe.

Katika kesi hiyo, upande wa mashitaka (Jamhuri), uliongozwa na wakili mwandamizi wa serikali, Neema Ringo, wakili wa serikali Prudence Rweyongeza na wakili mwingine wa serikali Janeth Sekule.

Upande wa utetezi, uliongozwa na wakili wa kujitegemea, Kamaliza Kayanga, Merdad Mutogole na Jacob Somi.

Kesi nyingine zitakazoanza kusikilizwa leo mahakamani hapo ni namba 25 ya mauaji kama hayo ya mtoto Esther Charles (13) mkazi wa kijiji cha Shilela, Kata ya Segese, Tarafa ya Msalala yaliyotokea Oktoba, mwaka jana inayowakabili washtakiwa watano ambao ni Masumbuko Madata na Charles Kalamuji au Charles Masangwa na Merdad Maziku Machunda mkazi wa mjini Kahama, Malalija Jitunga maarufu kama Katare na Peter Malima maarufu kama Mugabe wote wakazi wa wilayani Kahama.

Kesi nyingine ni nambari 26 ya mauaji ya imani za kishirikina ya kikongwe Ng’wana Gimbishi (75) inayomkabili mkazi wa kijiji cha Kagongwa, Kata ya Isagehe wilayani Kahama, Joseph Lugata yaliyotokea Januari 8, mwaka huu katika kijiji cha Kilimbu, Kata ya Mwaluguru wilayani hapa.

Mshtakiwa anadaiwa kumuua marehemu huyo kwa kukusudia.


1 comments:

Unknown said...

Let the justice be done

Post a Comment

 
BONYA HAPA