
Wakenya mbalimbali wamepinga hatua hiyo huku wakiishutumu tume hiyo kwa kuzembea na kwamba haina lolote la kujivunia.
Wakili Paul Muite ni mmoja wa wanasiasa ambao wamepinga uteuzi wa tume hiyo akisema, "Jaji Ringera ameshindwa kupambana na ufisadi nchini."
Rais Kibaki aliingia madarakani mwaka wa 2002 na kuahidi Wakenya kwamba serikali yake italivalia njuga zimwi la ufisadi.
Lakini amekosolewa na wengi ikiwa ni pamoja na nchi wafadhili ambao wanadai hakuna lolote lililobadilika kuhusu vita dhidi ya ufisadi.
Mshahara mnono
Licha ya kuwepo na madai dhidi ya vigogo kadha serikalini, hakuna yeyote ambaye amechukuliwa hatua.
Bwana Muite alidai kwamba uteuzi wa Jaji Ringera na wenzake ulikiuka sheria kwa kuwa bunge halikuhusishwa kama inavyopaswa.
Mwenyekiti wa bodi inayosimamia uteuzi wa tume hiyo, Okong'o Omogeni alielezea masikitiko yake kuhusu hatua ya Rais Kibaki.
Jaji Ringera ndiye mtumishi wa umma ambaye analipwa mshahara mnono wa dola elfu 34 kila mwezi.
Kiwango hicho ni kikubwa kuliko kile anacholipwa kiongozi wa nchi.
Jaji Ringera mwenyewe amekataa kujibu lolote kuhusu shutuma dhidi yake na tume anayoiongoza kupambana na ufisadi.
0 comments:
Post a Comment