TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, September 24, 2009

BREKING NYUUUUUZZZZZZZZZ: BOMU LAUWA WATTOTO WAWILI MBAGALA

4:10 PM

mpiga picha akifotoa sehemu ulipotokoea mlipuko wa bomu na kuua watoto wawili nan kujeruhi wengine watatu leo mbagala kizuiani jijini Dar.
mpiga picha selemani mpichi wa guardian akifotoa watoto wawili walionusurika na mlipuko wakiwa na mama wa jirani kwani mama yao ameenda hospitali kumhudumia majeruhi
majirani wakiwa wamemzunguka mama jirani na watoto waliojeruhiwa
Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh. William Lukuvi na kamanda wa Polisi wa Mkoa maalumu wa kipolisi afande Selemani Kova wakipata maelezo toka kwa Mkuu wa Wilaya Mh. Rugimbana mara baada ya kuwasili hospitali ya Temeke leo.

Habari za uhakika zilizoifikia Glob ya Jamii hivi punde zinaeleza kuwa Watoto wawili wamekufa kwa bomu huko Mbagala Kizuiani karibu na kambi ya Jeshi, wilaya ya Temeke, jijini Dar.
watoto waliofariki ni Regina Chawala (6) na Rajab Said (6) ambapo katika mlipuko huo pia kulikukuwepo na majeruhi watatu ambao ni mtoto Sada Seleman (2)Asha Seleman (5) pamoja na Stella Christian Chawala ambaye amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali ya Muhimbili kitengo cha wagonjwa mahututi.

Chanzo cha Mlipuko huo kimetajwa kuwa ni mabaki ya mabomu kufuatia mlipuko katika kambi ya Jeshi hivi karibuni. Jirani na eneo la tukio palikuwa na taka ambazo zinachomwa moto chini ya migomba, ndipo mlipuko ukasikika na watoto watano wote wakatupwa huku na kule, ambapo mmoja alifia hapo hapo na mwingine alipoteza uhai akiewahishwa hospitali ya Temeke.


Mkuu wa mkoa wa Dar Mh. William Lukuvi pamoja na kamanda Selemani Kova ambao walifika hospitali ya Temeke, wamesema kuwa ni kweli tukio hilo limetokea na ni bahati mbaya kwa kilichotokea na kwamba taratibu mbalimbali zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na mazishi na kuwatibu wajeruhia. Mh. Lukuvi amesema serikali iragharamia kila kitu.

1 comments:

Simon Kitururu said...

Hapa sasa kuna uzembe!

Kwa hiyo inamaana jeshi letu hata halijui lina mabomu mangapi na yako wapi kama inaweza kufikia mpaka kutojua uwepo wa mabomu haya mpaka yaue?

Mungu awalaze pema Marehemu!:-(

Post a Comment

 
BONYA HAPA