TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, September 24, 2009

Denti wa Sekondari Dar azama baharini, kufariki

11:32 PM

Kijana Shaaban Ali, 17, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Boko amefariki dunia kwa kunywa maji mengi wakati akiogelea katika Bahari ya Hindi.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mark Kalunguyeye, amesema tukio hilo limetokea mishale ya saa 3:30 asubuhi katika eneo la Kawe Beach Jijini Dar es Salaam.

Kamanda Kalunguyeye amesema kaka wa marehemu aitwaye Ali Juma, 33, ameiambia Polisi kuwa yeye na mdogo wake, mishale ya saa 10:00 jioni, walikwenda ufukweni hapo kwa nia ya kuogelea.

Akasema kwa mujibu ya maelezo ya kaka huyo wa marehemu, wakati wakiogelea, mdogo wake alizidiwa maji akazama na kunywa maji mengi kabla ya kufariki dunia.

Akasema mwili wa marehemu haukuonekana hadi jana mishale ya saa 3:30 ulipopatikana ukielea kando ya ufukwe huo wa bahari ya Hindi.

Kamanda Kalunguyeye amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mwananyamala.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA