MABINGWA wa soka wa Tanzania Bara, Yanga leo inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) utakaochezwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Yanga itatumia mchezo huo kama sehemu ya bonanza lake la kutambulisha jezi zake mpya itakazozitumia msimu huu ugenini na nyumbani.
Mkurugenzi wa kampuni ya CXC, Charles Hamka ambayo ndiyo waandaaji wa mchezo huo na bonanza zima la Yanga, alisema wameona vyema mabingwa hao wa soka Tanzania kupata michezo ya nguvu ya kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu nsimu ujao.
“Ni kama Simba walivyofanya, watatambulishwa wachezaji sambamba na jezi za timu za mechi za nyumbani na ugenini.
0 comments:
Post a Comment