TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, August 14, 2009

3:17 PM
HATIMAYE MADEREVA WA MABASI YA MIKOANI WASITISHA MGOMO
Baada ya kikao cha pamoja baina ya viongozi wa mkoa na viongozi wa madereva wa mabasi yaendayo mikoani, hatimaye safari za kwenda mikoani zimeanza kwenye majira ya saa nne.

Safari za mikoani zilikwama leo asubuhi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi baada ya madereva kugoma kufanya kazi, kama hatua ya kupinga adhabu aliyopewa dereva mwenzao aliyekuwa akiendesha basi la Mohhamed lifanyalo safari za Dar - Singida.

Dereva huyo alihikumumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela kufuatia ajali iliyolihusisha basi moja la kampuni ya Mohammed na lori iliyotea mkoani Tanga hivi karibuni.

Haijafahamika bado makubaliano yaliyoafikiwa katika kikao hicho kilichodumu kwa muda wa masaa matatu , lakini inaonekana kiasi flani cha makubaliano kimeafikiwa, hivyo kupelekea kuanza tena kwa safari za mikoani kituoni hapo.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA