Serikali ya Taiwani imetuma askari zaidi ya 4000 kuongeza juhudi za uokoaji huko maeneo ya kusini kuliko athiriwa na kimbunga, ambapo maji yanyoendelea kujiskusanya yakisababisha tishio jipya kwa vijiji ambavyo vilinusurika na kimbunga cha kwanza cha Morakot. Serikali imethibistisha, vifo zaidi ya 100 vimetokana na Morakot ambacho kimetiririsha mvua zaidi ya mita 2 kisiwani humo mwishoni mwa wiki iliyopita, kikiwakumbusha watu mafuriko makubwa yaliyowahi tokea miaka 50 iliyopita.
Mpaka sasa watu wapatao 108 wameshauawa na mafuriko hayo, lakini idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka.
Helikopta zilikuwa zikitafuta maeneo ya kusini mwa Taiwan na kuwaangushia vyakula kwenye vijiji ambavyo vimejitenga kutoka na barabara za kufikia huko kuharibiwa na mmomonyoko wa ardhi.
Watu karibia 14,000 wamehamisha kwa njia ya helokopta kupelekwa kenye usalama tangu mwishoni mwa wiki
Lakini walionusurika na wanasiasa wanaishutumu serikali kwa kuchelewa kidogo kwa shughuli hizo za uokoaji. Mwanakijiji mmoja alisema "hatukusaidiwa, tulisahaulika, tulikuwa tunasubiri helikopta bila kitu chochote"
0 comments:
Post a Comment