TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, August 25, 2009

Sitta aitaka jamii kukemea kauli za uongo

12:18 PM

Spika wa Bunge, Samuel Sitta, amewaasa jamii kukemea hulka ya kueneza kauli za uongo, kwa vile zinachangia kuigawa jamii na kujenga mazingira ya kuibua mifarakano.

Sitta alisema hayo juzi alipokuwa akihutubia katika tamasha la muziki wa Injili lililofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Ali Hassan Mwinyi mjini hapa.

Alisema katika siku za karibuni kumetokea tabia ya watu kuzusha uongo dhidi ya watu wengine, hali inayokatazwa pia kwenye misahafu ya dini.

Kwenye mkutano huo uliofurika maelfu ya wakazi wa mjini hapa, Sitta alikuwa mgeni rasmi na alitumia vifungu mbalimbali vya Biblia kukemea vitendo viovu na kuwahimiza watu kuishi kwa kufuata maadili mema.

Kwa upande wao, wachunguji mbalimbali kutoka Umoja wa Makanisa mkoani Tabora, walimuombea dua Sitta, ili adumu katika ukweli na kutetea maslahi ya wananchi walio wengi bila woga.

Naye Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margareth Sitta, alisema watu wanapaswa kutambua kwamba kila nafsi duniani itaonja mauti, hivyo kifo ni zawadi ya Mungu na kwamba kuishi ni majaliwa.

Waziri huyo ambaye ni mke wa Spika Sitta, alisema hayo wakati akikariri mafundisho ya Askofu Mkuu Robert Mtega wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Songea, alipohubiri kwenye mazishi ya mama wa Mbunge wa Perahimo, Jenista Mhagama.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA